MAUAJI YAENDELEA NYAMONGO
Wavamizi { intruders} wakijaribu kupambana na maaskari polisi na walinzi wa kampuni YA ABG NORTH MARA nyamongo tarime |
Watu wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi na jeshi la polisi kanda maaluum ya Tarime na Rorya kwa tuhuma ya kuvamia mgodi wa kuchimba Madini ya dhahabu wa barrick North Mara uliopo nyamongo wilayani Tarime Mara
Akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya tarime na rorya ACP Justus Kamgisha ameeleza kwamba mnamo tarehe 30/08/2012 kuanzia mida ya saa 12 jioni hadi saa moja jioni watu wanao kadiliwa kuwa kati ya 800 au 1000 kwa jina maarufu intruders walivamia mgodi wa ABG North Mara uliopo katika vijiji vya kewanja na nyangoto maeneo la rampad na shimo la Gokona wakiwa na slaa za jadi kama vile mapanga nyundo mawe na rungu wakiwa na nia ya kupora dhahabu na kuwashambulia askari polisi walio kuwa doria katika maeneo hayo
Kamanda kamgisha ameeleza kuwa katika jitihada ya kuwazuia wavamizi hao askari na E6059 D /COPLO JULIUS alikatwa panga usoni na na mgongoni na kuanguka ndipo askari wengine katika jitihada za kumuokoa askari huyo wavamizi {INTRUDERS} wawili PAUL SARYA miaka 26 wa wa kiji cha nyangoto na RODGERS MWITA miaka 18 wa kijiji cha kimusi walipigwa Risasi na kufariki
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya tarime DR Nega Marco amekiri kupokea maiti wawili na majeruhi mmoja ambae ni Mseti Chacha miaka 20 mkazi wa nyamwaga
Pia jeshi la polisi kanda maalum ya tarime rorya imetoa rai kwa wananchi kwa kuwataka watii sheria bila shuruti kwa kuacha kuvamia mgodi huo kwa nia ya kupora mawe yenye dhahabu
tabia na vitendo vya kuvamia mgodi wa abg north mara vimekuwa vikijirudia mara kwa mara na kusababisha baadhi ya wananchi wengi kupoteza maisha wakiwemo raia, walinzi wa mgodi na baadhi ya askari polisi kujeruhiwa vibaya na wavamizi {INTRUDERS} ni vyema sasa serikali ikaangalia upya nanma ya kusaidia na kutatua tatizo hili linalogusa zaidi wananchi wa wilaya ya tarime na watanzania wote kwa ujumla..
Maoni
Chapisha Maoni