WACHIMBAJI WAIOMBA SERIKALI MKOPO NA VIFAA

NA JUMANNE NTONO - TARIME MARA

Wachimbaji wadogowadogo  wanao fanya shughuri zao katika maeneo yanayo zunguka mgodi wa kuchimba madini ya  dhahabu barrick north mara uliopo nyamongo wilayani tarime mkoa wa mara wanaiomba serikali iwasaidie vifaa vya kujikinga na madhara ya zebaki [mercury} wakati wanapo wosha dhahabu 

wakiongea na wandishi wa habari walipo watembelea katika maeneo yao ya kazi. wachimbaji hao wameeleza kwamba kwa sasa wanaosha dhahabu bila kinga yoyote

Na pia wameeleza kwamba wengi wao hawajui madhara ya zebaki kutokana na  kuto kuwa na elimu ya kutosha kuhusu madhara hayo' kwa hiyo wenaiomba serikali iwasaidie vifaa vya kujikinga na madhara hayo  ikiwa ni pamoja na mipira na viatu vigumu aina ya buti

kutokana na maomba hayo mkuu wa wilaya ya tarime Bw John Henjewere ameeleza kwamba serikali ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo watakao kuwa wamesajiliwa tu. kwa hiyo amewahasa Wachimbaji hao wajiunge kwenye vikundi na wavisajiri.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KIJIJI CHA KERENDE CHAKABIDHIWA BARABARA YA TSH MILIONI 26-TARIME

MAUAJI YAENDELEA NYAMONGO

VIONGOZI WANAO HAMASISHA KILIMO CHA BANGI KUCHUKULIWA HATUA