JESHI LA POLISI LATAKIWA KUWATENDEA HAKI WAANGA WA LIO TENDEWA VITENDO VYA UKATIRI WA KIJINSIA
ASKARI POLISI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO YA KUPINGA VITENDO VYA UKATIRI WA KIJINSIA -TARIME MARA
Ikiwa ni hitimisho la siku 16 za maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia  hapa Tanzania  jeshi la polisi wametakiwa kuepuka lugha chafu ,kejeli,na vishawishi vya rushwa kwa waanga au walio tendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia

Hayo yameelezwa na askofu wa kanisa la anglikana dayosisi ya Tarime DR MWITA AKIRI kwenye ufunguzi wa ofisi ya dawati la jinsia na watoto la kituo cha polisi  wilaya ya tarime mkoani mara

DR MWITA AKIRI amewataka askali polisi wote watakao Kuwa katika ofisi ya dawati la jinsia na watoto wawe watu wa msaaa kwa waanga walio tendewa vitendo vya  ukatiri wa kijinsia ili wajenge imani kwa jamii kwamba dawati lililo anzishwa ni msaada kwa jamii siyo dawati la kuikatisha jamii tama ya  kupata haki yao

Na amewataka polisi waepuke  lugha chafu,kejeli,na vishawishi vya rushwa toka kwa waanga wa vitendo vya ukatiri kwa lengo la kupotosha haki zao

Kwa upande wake kaimu kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya  tarime na
 rorya  SSP SEBASTIANI  ZAKARIA  amewataka wananchi viongozi wa chama na serikali  na wadau wote ambao hawapendezwi na vitendo vya ukatiri wa kijinsia washirikiane na jeshi la polisi kuakikisha kama siyo kupunguza basi kumaliza kabisa vitendo vya ukatiri na unyanyansaji wa kijinsia katika wilaya ya tarime na Tanzania kwa ujumla

 Mapema akisoma lisara kwa mgeni  lasmi WP CHAUSIKU  alieleza lengo la kuanzishwa kwa ofisi ya  dawati la vitendo vya ukatiri wa kijinsia kwa wanawake na watoto

 Mpaka  sasa zaidi ya watoto wa kike 300 walio kuwa watarajiwa kukeketwa mwezi huu wa 12  wamekimbilia katika kituo cha tohara{ ukeketaji} mbadara cha kanisa la  romani kathoriki cha masanga kilichopo wilayani  tarime.

……………………………………. mwisho ……………………………………….



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KIJIJI CHA KERENDE CHAKABIDHIWA BARABARA YA TSH MILIONI 26-TARIME

MAUAJI YAENDELEA NYAMONGO

VIONGOZI WANAO HAMASISHA KILIMO CHA BANGI KUCHUKULIWA HATUA