NA JUMANNE NTONO – MUGUMU SERENGETI MARA
0786 992 552 / 0763 992 552 / 0715
992 552
Wakati zoezi la kukusanya maoni ya katiba likiendelea mkoani
mara wananchi wa wilaya ya Serengeti mkoani humo wameaswa kujitokeza kwa
wingi ili kutoa maoni yao
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa vijana wa chama cha
demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa
mara bw chacha heche wakati wa kufungua
ofisi ya tawi jipya la chadema katika stendi yaw mugumu
Bw chacha amewataka
wananchi hususani vijana waakikishe wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la
kukusanya maoni kwa wananchi ili watoe mawazo yawo ya msingi hususani tatizo la
ardhi ambayo imekuwa na migogoro mikubwa
hapa nchini na kusababisha baadhi ya
wananchi kuonekana kana kwamba ni wakimbizi katika nchi yao
Pia bw chacha ameeleza kwamba jukumu la kuleta maendeleo katika nchi hii nila kila
mwananchi kwa hiyo wananchi watoe maoni yao yanayo lenga
maendeleo ya watanzania ikiwemo kulejesha viwanda na mashirika ya umma yaliyo kufa kwa sababu ya uzembe wa watu wachache walioko
madarakani
Kwa upande wake diwani wa kata ya stendi kuu ya mugumu bw rioba
marwa amewaeleza wananchi kwamba madiwani
walio wachagua siyo wawakilishi wa wananchi bali niwafanya biashara walio
chaguliwa kufanaya biashara na halmashauli.
miradi mingi inayo tekerezwa katika halmashauli hiyo ina ubora wa chini na sii ya
kiwango kilicho kusudiwa. kwa sababu
tenda nyingi za miradi hiyo kuchukuliwa na madiwani wa halmashauli hiyo.
hali ambayo husababisha usimamiaji wa
miradi hiyo kuwa mgumu na ukizingatia wasimamizi na wakaguzi wa miradi hiyo ni
haohao madiwani wenye tenda.
Sambamba na ufunguzi wa tawi hilo chadema wanatarajia kufugua matawi mengi zaidi katika kila kata na kila kijiji wilayani
Serengeti.
Maoni
Chapisha Maoni