NA JUMANNE NTONO -
TARIME MARA
05/12/2012
0786 992 552 / 0763 992 552 / 0715 992
551
Wazee wa mila tarime wameyataka mashirika mbalimbali ya
yanayo toa elimu kuhusu kutokomeza
ukeketaji kwa mtoto wa kike tarime
yaache tabia ya kuwatumia kama vitega uchumi vyao na badara yake walete
mabadiriko kwa jamii
Hayo yalielezwa na viongozi wa wazee wa mila kutoka koo 13
za kabila la wakurya walio kuwa kwenye
mafunzo na majadiano ya kutafuta
ufumbuzi wa kutokemeza suala la ukeketaji
kwa watoto wa kike wilayani humo mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la
utu wa mtoto CDF
Wazee hao wamekuwa na
ofu na kusababisha wadai kwamba pengine baadhi ya mashirika yanayo kuja
kuielimisha jamii kuhusu jambo hilo na kuwaita watu wachache katika kumbi za mjini wakiwemo
wazee wa mila wachache yanawatumia wazee hao kama mitaji yao ya kuombe pesa
kutoka kwa wafadhiri mbalimbali wanao wasaidia lakini siyo kuja kumaliza
tatizo la ukatiri kwa mtoto wa kike
Kwa upande wake mkuu
wa wilaya ya tarime bw john henjewele ameeleza kwamba pamoja na kutoa mafunzo
mbalimbali kuhusu madhara ya ukeketaji kwa jamii. serikali kupitia halmashauli ya wilaya ya tarime kwa sasa wana tarajia
kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana
katika kijiji cha borega kuanzia kidato
cha kwanza hadi cha sita wilayani tarime
Pia mkurugenzi wa shirika la utu wa mtoto[ cdf] bw konshuma mtengeti. Amesema kwamba pamoja na changamoto
zinazo wakabili . kupitia shirika lao wataendelea kuisapoti jamii katika kutoa
elimu kuhusu madhara ya ukeketaji kwa
mtoto wa kike na amewaomba wananchi
viongozi wa chama na serikali
waendelee kuwapa ushirikiano katika masuala ya ukeketaji kwa mtoto wa
kike.
Na katika kipindi hiki cha mwezi wa kumi na mbili zaidi ya
koo kumi kati ya koo kumi na tatu za kabila la wakurya wilayani tarime wanatarajia kukeketa watoto wa kike zaidi ya
miatatu
Maoni
Chapisha Maoni