NA JUMANNE NTONO
0786 992 552/ 0763
992 992/ 0715 992 552
12/12/2012
Umoja wa makanisa ya kikristu tanzania cct na watoto wa kike
wametoa tamko la kukataa ukeketaji
wilayani tarime
Tamko hilo limetolewa na mkuu wa dayosisi ya Tarime kanisa la menonite tanzania mchungaji
ANDREW RYAGA kwa niaba ya cct wilaya ya
Tarime na watoto wa kike katika
kongamano la kukataa na kupinga vitendo
vya kikatiri na vya unyanyasaji kwa watoto wa kike lililo
fanyika katika kijiji cha Kemakorere wilayani Tarime
Wakitoa tamko hilo mchungaji ANDREW RYAGA
amesema kwamba mtu yoyote atakae bainika akijiusisha na vitendo vya
ukeketaji kwa watoto wa kike mwaka huu
achukuliwe hatua kwa kukeuka agizo la serikali na madhehebu yote ya dini ya kikristo Tanzania.watoto wa
kike nao wakawataka viongozi wa serikali watoe agizo kwa wale wanao keketa watoto wa kike kama walivyo toa agizo kwa
walio jiusisha na ukatwaji wa viuongo vya walemavu wa ngozi Maalbino
Nao baadhi ya wazazi walio hudhuri tamasha hilo lililo
shirikisha zaidi watoto wa kuanzia miaka
tisa hadi kumi na tano ambao wengi wao
ndio wanarengwa kukeketwa kwa kipindi hiki cha mwezi wa 12 mwaka huu wao
wameitupia serikali lawama kwa kushindwa kuwachulia hatua za kisheria wale wote
wanao jihusisha na vitendo vya ukeketaji huku wakiwaona kwa macho yao wakifanya sherehe za ukeketaji kwa watoto
wa kike
Kwa upande wake mgeni rasmi wa tamasha hilo
katibu tarafa wa tarafa ya inchage wilayani tarime BW JONATHAN MACHANGO
amewaeleza wananchi kuwa badara ya kuchangia sherehe kwa ajiri ya ukeketaji kwa
mtoto wa kike sasa wachangie elimu kwa watoto hao ili wapate elimu itakayo
wasaidia katika maisha yao
ya badae
Mapema mratibu wa tamasha hilo mchungaji JOSEPH MAHUGIJA
alieleza kwamba lengo la tamasha hilo ni kutoa elimu kwa jamii ili iachane na vitendo vya ukatiri wa kijinsia kwa
wanawake na watoto.
Maoni
Chapisha Maoni