michezo
Hatimae timu ya polisi tarime mkoani mara imeibuka bingwa
wa ligi ya amani mahusiano cup kwa mpira wa miguu na wa pete
Timu hiyo ya polisi iliyo ingia fainali na timu ya kijiji
cha matongo imeibuka bingwa wa mpira wa miguu kwa wanaume kwa kuifunga magori matatu kwa bila pia imekuwa
bingwa wa mpira wa pete kwa wanawake kwa kuifunga timu ya sodesco kwa magori 42
kwa 5
na baada ya fainali hizo kumalizika katika viwanja vya sekondari ya nyamongo makocha wa timu za polisi walisema kwamba siri
ya ushindi wao ni maandalizi mazuri ya timu zao na ushirikiano mzuri kutoka kwa
uongozi wa timu walimu na wachezaji
huku kocha wa timu ya
matongo BW JOSEPH MTOTO akieleza kwamba
timu yake imeshindwa kutwa kombe hilo
kwa sababu ya wachezaji wake kuogopa jina la polisi
kwa upande wa wadhamini wa mashindano hayo shirika la search for common ground lililopo
tarime na kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu
ya African barrick gold{ north mara}wamewapongeza wananchi kwa
ushirikiano walio utoa na namna walivyo hamasika na kuonyesha ushirikiano katika suala zima la
kujenga mahusiano kwa njia ya michezo
na wakaeleza kwamba lengo la mashindano hayo ni kuwaweka
pamoja wadau mbalimbali kwa njia ya
michezo ambao kwa njia nyingine wana muingiliano wa moja kwa moja na shughuli
za uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo la nyamongo baina ya polisi jamii
mwekezaji na serikali ili kujadili na kukumbushana wajibu wa kila mmoja wao
kutambua tofauti zao na kuishi kwa makubaliano
katika mashindano hayo mshindi wa kwanza mpira wa miguu aliibuka na kikombe mipira 4
na shilingi laki nane huku mshindi wa kwanza mpira wa pete akiibuka na
kikombe mipira mine na shilingi laki tatu.
ligi hiyo ilishirikisha timu 40 za michezo mbalimbali
ikiwemo bao’ draft’ kufukuza kuku’
kuvuta kamba’ na kukimbia na maji kichwani
NAHODHA WA TIMU YA POLISI TARIME MPIRA WA MIGUU AKIPOKEA MOJA YA ZAWADI WALOZO PEWA |
NAHODHA WA TIMU YA POLISI TARIME MPIRA WA PETE BI NYAMINGA AKIPOKEA KIKOMBE CHA UBINGWA WA AMANI MAHUSIANO -NYAMONGO |
Maoni
Chapisha Maoni