WAZIRI WA KAZI NA AJIRA MH GAUDENSIA KABAKA AKIWAKABIDHI ZAWADI WAHITIMI 13 WA MAFUNZO YA TOHARA MBADARA WA KITUO CHA MASANGA WILAYANI TARME MARA |
WAHITIMU 13 WA MAFUNZO MBADARA YA TOHARA AU UKEKETAJI WAKIIKMBA NYIMBO ZA FURAHA |
Watakao vamia kituo cha kutoa elimu ya tohara mbadara kwa
watoto wa kike cha masanga wilayani tarime mkoani mara kwa nia
yakuvuruga Marengo ya kituo hicho watashughulikiwa
na serikali
Agizo hilo
limetolewa na waziri wa ajira na kazi BI
GAUDENSIA KABAKA
Kwenye sherehe ya kuhitimu mafunzo ya elimu mbadara ya ukeketaji kwa watoto wa kike iliyo fanyika katika kituo
cha masanga wilyani tarime
BI GAUDENSIA amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya kuakikisha walimu na watoto wote wa kike wanao pata
elimu mbadara ya ukeketaji katika kituo cha masanga wanaishi kwa amani bila
vitisho vyovyote kutoka kwa wananchi wa eneo hilo
Pia mh gaudensia
ameiomba kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu AFRICAN BARRICK GOLD NORTH MARA
iliyopo nyamongo wilayani tarime pamoja na majukumu makubwa waliyo nayo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya huduma za jamii. kama
upo uwezekano basi ni vyema wakajengewa chuo cha ufundi katika mkoa wa mara ili kunusuru vijana wengi wa mkoa huo wanao hitaji
kujiendeleza katika fani mbalimbali za
ufundi
Mapema akisoma risala ya chuo kwa mgeni rasmi BI EUNICE ANTHONY amesema kwamba wao hawana kituo cha kuhifadhi watoto wanao
kimbia kukeketwa bali wana kituo cha kufundisha elimu mbadara ya ukeketaji inayo
mfanya mtoto wa kike aweze kujitambua kimwiri na kiakili.
Watoto wa kike nao
kupitia risala yao wameitaka serikali iwachukulie hatua kali
wazazi wanao watendea watoto wa kike vitendo vya ukatili
Toka mwaka 2008 hadi 2012 jumla ya watoto wa kike 642
wamehitimu mafunzo ya tohara mbadara katika kituo hicho na kukabidhiwa kwa wazazi wao, huku wazazi hao
wakitakiwa kuto wafanyia vitendo vyovyote vya kikatiri majumbani mwao.
HAWA NI BAADHI TU YA WATOTO WA KIKE WANAO ENDELEA KUPATA ELIMU YA TOHARA MBADARA KATIKA KITUO CHA MASANGA |
Maoni
Chapisha Maoni