KIJIJI CHA KERENDE CHAKABIDHIWA BARABARA YA TSH MILIONI 26-TARIME
KAIMU MENEJA WA KAMPUNI YA ABG NORTH MARA BW MARC LUTY AKIKATA UTEPE WA BARABARA NA KUKABIDHI KWA M/KITI WA KIJIJI CHA KERENDE-TARIME |
WANANCHI WA KIJIJI CHA KERENDE NA VIONGOZI WA ABG NORTH MARA WAKIKAGUA BARABARA |
Katika harakati za kujenga mahusiano mazuri na jamii inayo zunguka mgodi wa dhahabu wa NORTHI MARA. Kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu ABG NORTH MARA iliyopo nyamongo wilayani tarime mkoani mara imekamilisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa moja na nusu yenye thamani ya shilingi milioni 26 za kitanzania na kuikabidhi kwa uongozi wa kijiji cha kerende wilayani humo
Akikabidhi barabara hiyo kaimu meneja wa kampuni hiyo BW MARC LUYT amesema kwamba kampuni imejenga barabara hiyo kwa maombi maalum yaliyo letwa na uongozi wa kijiji hicho kwa kuona kwamba ndicho kipaumbele chao wanacho kitaka, kampuni iwasaidie.
Pamoja na kujenga barabara hiyo kaimu meneja wa kampuni hiyo BW MARC LUTY amesema kwamba lengo la kampuni ni kuakikisha inajenga mahusiano mazuri baina ya wananchi na kampuni kwa kutekereza miradi yote ya maendeleo waliyo kubaliana na wananchi wa vijiji vinavyo zunguka mgodi huo
Akipokea msaada huo mwenyekiti wa kijiji cha kerende Bw Mambeka Mohamed ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwajengea barabara hiyo na ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa kampuni hiyo pale atakapo kuwa anahitajika kushirikiana nao
Kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa barabara hiyo wameeleza kwamba kukamilika kwa barabara hiyo ni neema kwao. Kwa sababu hata wakiuguliwa nyakati za usiku ni rahisi kufika katika hosipitali kwa ajiri ya kupata huduma.
Hata hivyo kampuni ya ABG NORTH MARA iliisha anza kuitekereza na inaendele kutekereza miradi kwa wananchi wa vijiji vinavyo zunguka mgodi huo ujenzi wa barabara,ujenzi wa shule ,huduma za afya na maji.
WAKATI Serikali inaendelea kupiga marufu biashara na kilimo cha zao haramau la bangi, kwa kufyeka mashamba ya zao hilo na kuwakamata wakulima wafanya biashara na watumiaji wa zao hili na wengine wakifikishwa mahakamani, bado hatua hizo za serikali zinaonekana si chochote kwa wananchi wa wilaya yaTarime kwani bado kilimo cha zao hili kinazidi kushamiri katika maeneo kadhaa, huku zao hilo wakiliita dhahabu ya kijani.
JibuFutaHali hiyo imedhihilika baada ya kuanzishwa kwa opresheni ya tokomeza bangi tarime inayo ongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Glorious Luoga ambayo kwa mda mfupi imeteketeza zaidi ya ekari 80 ya mashamaba ya bangi katika maeneo kadhaa wilayani tarime.
pamoja na kuteketezwa kwa mashamaba hayo ya bangi bado baadhi ya wananchi wanadai kwamba hawataweza kuacha kulima zao hilo kwa kuwa hawajaona kama kuna zao mbadala linalo weza kuwapatia kipato kama ilivyo kwa zao hili la bangi