Hizi ni baadhi ya nyumba zilizo kabidhiwa kwa uongoizi wa shule ya sekondali ya ingwe- Tarime |
kushoto kaimu meneja wa NORHI MARA Bw MARCK LUYT na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauli ya wilaya ya Tarime Bw Athuman Akalama wakikata utepe na kukabidhi nyumba 12 kwa shule ya sekondali Ingwe- Tarime |
Kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu ya ABG NORTH MARA iliyopo nyamongo wilayani tarime mkoani mara
imekamilisha ujenzi wa nyumba kumi za kuishi zenye thamani ya shilingi milioni
685 za kitanzani na kukabidhi kwa
uongozi wa shule ya sekondali ingwe iliyopo nyamongo wilayani tarime
Akikabidhi nyumba hizo kwa mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauli ya wilaya ya Tarime Bw Athumani Akallama kaimu meneja wa kampuni
hiyo BW MARC LUYT ameelza kwamba lengo la kampuni ni kuhakikisha
inashirikiana na wananchi katika kuboresha huduma ya jamii hususani upande
wa elimu
Akipokea msaada huo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauli ya wilaya
ya tarime BW Athumani Akallama
ameipongeza kampuni hiyo na kueleza kwamba kampuni hiyo imesaidia mambo
mengi katika wilaya hiyo katika sekta ya
elimu barabara afya na maji Na akawataka wananchi wa wilaya hiyo waendelee
kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo na
kutunza miradi yote inayo tekerezwa na kampuni hiyo.
Bw Tanzania Omtima
ambae ni mwenyekiti wa kijiji cha kewanja na Bw Wilson Mangule
diwani wa kata ya kemambo pamoja na kuishukuru kampuni hiyo kwa kuwajengea
nyumba kumi za walimu. wameitaka kampuni hiyo iendelee kuisaidia shule
hiyo kwa kuwajengea uzio katika shule
hiyo na kuwawekea umeme ili kunusuru wanafunzi wengi wanao kumbana na
vishawishi vya pesa nyingi inayo
toka katika mgodi huo wa NORTH MARA
Kampuni hiyo inaendelea na ujenzi vyumba vinnne vya mahabara katika shule hiyo ikiwa
na lengo la kuboresha shule hiyo kuwa ya kisasa zaidi ikiwezekana iwe shule ya
mfano katika mkoa wa mara.
………………………………..mwisho…………………………………………………….
vingozo wakiangalia nyumba zilizo kabidhiwa kwa uongozi wa shule ya sekondali ingwe - Tarime |
Maoni
Chapisha Maoni