NEW LIFE CHRIST WAENEZA INJIRI MARA
Ili kupunguza mambukizi mapya ya virusi vya ukimwi wilayani Rorya mkoani Mara wananchi wametakiwa kuepukana na mira potofu na kumrudia mungu
Wito
huo umetolewa na mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kikristo mkoa wa dar es salaam mchungaji HALSON MUMANYI kwenye hitimisho la mahubiri ya
siku nane yaliyo endeshwa na shiriks la NEW LIFE CHRIST katika wilaya ya Tarime na Rorya mkoani Mara
Mwenyekiti Halson
ameeleza kwamba wilaya ya Rorya inamaambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi
kutoka na wananchi wengi wa wilaya hiyo kuto mrudia mungu
Pamoja na watu kumrudia mungu mwenyekiti huyo amewataka
wananchi wa wilaya ya Rorya na Tarime
waache tabia ya kurithi wake wa marehemu
{ wajane} kwa madai kwamba
wanadumisha mira, kwa kuwa mira hiyo imepitwa na wakati na haina tija tena kwa jamii
Nao baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali walio
hudhuria mahubiri hayo wamesema kwamba mahubiri ya siku nane yatawaimarisha kiroho
Kwa takwimu za mwaka 2012 wilaya ya rorya ni ya kwanza kimkoa
kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 6.2
………………………mwisho…………………………………….
Maoni
Chapisha Maoni