DC NA MBUNGE WAONDOA TOFAUTI ZAO WAJIKITA KATIKA MAENDELEO- RORYA
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN GABRIEL TUPA AKIONGEA KWENYE KIKAO CHA USURUHISHI KATIKA UKUMBI WA SOHA HOTEL UTEGI RORYA |
TUPA AMALIZA MGOGORO WA DC NA MBUNGE- RORYA]
Hatimae mgogoro mkubwa wa kutoelewana kwa viongozi wawili wa ngazi ya juu katika wilaya ya rorya mkoani mara ulio kuwa umeibuka hivi karibuni na kusababisha kukwama kwa shughuli za maaendeleo kwa wananchi huku wananchi wakibaki na kitendawili cha sintafahamu hatimae umemalizika
DC wa Rorya Elias Goroi akiongea katika mkutano wa kikao cha usuruhishi |
Viongozi hao ambao ni mkuu wa wilaya ya rorya bw Elias Goroi na mbunge wa jimbo hilo bw Lameck Airo kwa pamoja na mbele ya kikao kilicho itishwa na mkuu wa mkoa mara bw John Gabriel Tupa katika mji mdogo wa utegi na kushirikisha wazee maarufu wa wilaya rorya na viongozi wa madhehebu ya dini viongozi hao wameondoa tofauti zao na kusem kwamba watashirikiana kwa pamoja katka kuijenga Rorya
Kitendo cha viongozi hao kukubaliana na kuondoa tofauti zao kimepongezwa na wazee na vingozi wa dini na kuwataka waliyo yasema yawe yametoka moyoni mwao kama walivyo tamka wenyewe alisema mzee Kembo Migire na askofu wa kanisa la mennonite John Nyagwegwe
kushoto Lameck Airo mbunge rorya akiongea kwenye kikao cha usururhishi wa mgogogro wa dc na mbunge |
Akifunga kikao hicho mkuu wa mkoa wa mara bw John Gabriel Tupa ametoa wito kwa viongozi wote wa mkoa mara wawe na tabia ya kuwa na vikao vya mara kwa mara vitakavyo wasaidia kubaini baadhi ya changamoto zinazo wakabili na kuzitatua kwa wakati bila marumbano
Maoni
Chapisha Maoni