05/ 12/2013
[MTU MMOJA AUAWA KWA
KUPIGWA RISAS I- TARIME]
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
la John Chacha Mwita mkazi wa kijiji cha Bonchugu wilaya Serengeti mkoani Mara ameuawa kwa
kupigwa risasi shingoni katika maeneo ya
kijiji cha nyakunguru karibu na mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu wa ABG North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara
Tukio hilo lilitokea majira
ya saa tatu usiku ambapo Baadhi ya
wananchi walio shuhudia wameeleza kwamba
mtu huyo ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa jeshi la polisi kanda maalum
ya Tarime /Rorya ambao walikuwa zamu ya kulinda eneo la mgodi wa ABG
North Mara na kuongeza kuwa marehemu alikuwa akielekea nyumbani kwake
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi
kanda maalum ya Tarime na Rorya ACP
Swetberty Njewike amekiri kutokea kwa tukio hilo Tarehe 03 / 12 / 2013 saa tatu usiku lakini jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini muhusika, Pamoja na wananchi kudai kwamba mtu huyo
ameuwawa kwa kupigwa risasi na Askari wa
jeshi la polisi.
Matukio haya yanasababishwa na Mahusiano
mabaya kati ya wananchi wa vijiji
vinavyo zunguka mgodi wa dhahabu wa ABG North Mara na askari wa jeshi la polisi walio pewa
dhamana ya kulinda mgodi huo yamekuwa si
mazuri na kusababisha vurugu za mara kwa mara katika eneo hilo .
MWISHO
Maoni
Chapisha Maoni