[KANISA LA KKKT LALAANI MAUAJI TARIME}
Kanisa la kiinjiri la kirutheri Tanzania dayosisi ya mkoani mara
limelaani mtu au kundi lililo fanya mauaji ya watu nane katika mji wa tarime na
kusema mungu hapendezwi na matukio ya haina hiyo na kwa kupitia maombi mtu au
watu walio fanya matukio hayo watabainika
Hayo yameelezwa na askofu wa kanisa la kkkt dayosisi ya
mkoani mara askofu Michael Adam
kwenye ibada ya mazishi ya daudi mwasi alie zikwa katika kijiji cha nyamwaga wilayani tarime , ambae ni mmoja kati ya watu 8 walio uawa usiku wa tarehe 27 january 2014 kwa kupigwa
risasi na watu au mtu asie julikana
Askofu Michael amesema kwamba
kwa ushirikiano wa maombi sala vyombo vya dora na raia wema ana amini
waharifu au mharifu huyo atakamatwa na
sheria kuchukua mkondo wake
Pia baadhi ya wananchi walio shiriki katika mazishi hayo
akiwemo mbunge msitaafu wa jimbo la tarime Charles
Mwera , diwani wa kata ya Nyamwaga
Wambura Nyagare na John
Rotente nao wamelaani mauaji hayo na
kuwataka wananchi watoe ushirikianao kwa jeshi la polisi katika kufanikisha
zoezi la kuwabaini wahusika wa matukio hayo
………………………………….MWISHO………………………………………
Maoni
Chapisha Maoni