NYUMBA
YATEKETEA KWA MOTO TARIME
NYUMBA
pamoja na vyombo vya ndani vya Naftari Philipo Akyoo mkazi wa mtaa wa bomani
katika Halmashauri ya mji wa Tarime mkoani mara imeteketea kwa moto unaodhaniwa
kuwa chanzo chake kimetokana na shoti ya umeme wa Tanesco
akiongea
katika eneo la tukio la nyumba kuungua moto,mmmiliki wa nyumba hiyo Naftari
Philipo Akyoo anasema kabla ya siku nne kutokea kwa tukio hili,alitoa taarifa ya
tatizo la umeme wa nyumba hiyo katika ofisi ya Tanesco wilaya yaTarime na
wakafika kuona tatizo, lakini kabla ya kuja kutatua tatizo hili ,nyumba ikawa
Tayari imeungua
nao baadhi
ya mashuhuda wa tukio hili ambao ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa bomani Marema
Solo, na diwani wa kata ya bomani Godfrey Masubo,wao wakaelekeza lawama zao kwa uongozi wa Halmashauri ya mji
wa Tzarime kwa kushindwa kununua gari la
zima moto
wilaya ya
Tarime inao askari wa jeshi la zima moto lakini jeshi hili halina gari la
kuzima moto
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni