05/ 12/2013

[MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISAS I- TARIME]

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la John Chacha Mwita  mkazi wa kijiji cha Bonchugu  wilaya Serengeti mkoani Mara ameuawa kwa kupigwa risasi shingoni  katika maeneo ya kijiji cha nyakunguru karibu na mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu wa ABG North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara

Tukio hilo lilitokea majira ya  saa tatu usiku ambapo Baadhi ya wananchi walio shuhudia wameeleza  kwamba mtu huyo ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime /Rorya ambao walikuwa zamu ya kulinda eneo la mgodi  wa ABG North Mara  na kuongeza kuwa  marehemu alikuwa akielekea nyumbani kwake

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya ACP Swetberty  Njewike  amekiri kutokea kwa tukio hilo Tarehe 03 / 12 / 2013 saa tatu usiku  lakini jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini muhusika,  Pamoja na wananchi kudai kwamba mtu huyo ameuwawa kwa kupigwa  risasi na Askari wa  jeshi la polisi.  

Matukio haya yanasababishwa na Mahusiano mabaya kati ya wananchi  wa vijiji vinavyo zunguka mgodi wa dhahabu  wa ABG North Mara  na askari wa jeshi la polisi walio pewa dhamana ya  kulinda mgodi huo yamekuwa si mazuri na kusababisha vurugu za mara kwa mara katika eneo hilo.


MWISHO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KIJIJI CHA KERENDE CHAKABIDHIWA BARABARA YA TSH MILIONI 26-TARIME

MAUAJI YAENDELEA NYAMONGO

VIONGOZI WANAO HAMASISHA KILIMO CHA BANGI KUCHUKULIWA HATUA